Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Category | Child Protection |
Resource Owner | Chrissy Sykes |
Author | Chrissy Sykes |
Kitabu cha kazi cha watoto cha Mwili Wangu ni Mwili Wangu ni kitabu cha usaidizi, cha rasilimali kinachoingiliana na kilichoundwa kusaidia watoto kujihusisha na yaliyomo katika kipindi cha Mwili Wangu ni Mwili Wangu na video za muziki. Kitabu cha kazi kinafuata sauti na mlolongo wa hizo video, na hushugulikia uzuizi wa unyanyasaji wa watoto kwa njia chanya, na yenye rika inayofaa kupitia shuguli zinazo andaa watoto kujilinda mtu anapo watusi ama kutenda mabaya kwao. Haya mashuguli ya rika sawa yanasaidia watoto wawe na ujasiri, walinde mwili wao, watambue tabia za unyanyasaji, waelewe hisia zao na watambue watu wazima wanao weza kuzungumza nao kama mtu akijaribu kuwanyanyasa.
ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio katika mazingira hatarishi. Sisi ni jamii ya wafuasi wa Yesu duniani iliyojitolea kwa ajili ya ukuaji wa watoto katika ujumla. Tunakualika ujiunge nasi katika jamii hii yenye ushirikiano ili ushirikishe mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika shida.
ForChildren.com inatolewa na Compassion International, shirika lisilo la kujipatia faida lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na si kwa faida.