Kupitia uzoefu huu wa mafunzo ya mtandaoni, utapata ufahamu wa maadili na Biblia wa kwa nini ulinzi wa watoto ni muhimu na jinsi kulinda watoto kunakuza matokeo mazuri kwa watoto. Kwa ziada, wanafunzi watapokea maelezo kuhusiana na matarajio ya tabia mwafaka na tabia zisizofaa kwa watoto kulingana na Taarifa ya Kujitolea kwa Ulinzi wa Watoto na Kanuni ya Tabia ya Compassion.

Kozi hii ya mtandaoni ya mafunzo ya ulinzi wa watoto inajumuisha sera mahususi za Compassion na mbinu za ulinzi wa watoto. Hata hivyo, yaliyomo yanahusisha na yanapatikana kwa wanafunzi wote wanaojitolea kuangalia na kulinda watoto kama inavyoamrishwa na Yesu Kristo.

Mwisho wa kozi hii, wanafunzi wanatakiwa watie saini Taarifa ya Kujitolea, na wakubali kufuata matarajio ya tabia yaliyoorodheshwa kwenye kozi.


person taking picture of childLengo la mafunzo haya ni kuwapawanafunzi ufahamu na ujuzi wa kukabiliana na unyanyasaji wa watoto kingono mtandaoni (UWKM). Itarahisisha kutambua ishara na dalili za UWKM, kuelimisha walengwa juu ya madhara ya muda mrefu ya UWKM, Kuwasilisha mikakati ya kutekeleza na kuwasaidia wanafunzi kutambua namna mbalilmbali za kuwaponya wahanga katika mazingira yao.

Lengo la mafunzo haya ni kumwezesha mwanafunzi kuwa na taarifa naujuzi wa kushughuikia utelekezaji wa mtoto. Mafunzo haya yataimarisha namna ya kutambua dalili na ishara za utelekezwaji, itaelimisha wasikilizajikuhusu madhara ya muda mrefu ya utelekezaji, itawakilisha mbinu/mikakati ya kuingilia kati na itawasaidia wanafunzi kutambua rasilimali mbadala zilizoko kwenye eneo husika za kusaidia katika uponyaji wa mwathirika.

Lengo la Mafunzo haya ni kuwawezesha wanaojifunza wapate maarifa na stadi za kushughulika na Unyanayasaji wa mtoto Kihisia. Itasaidia kuimarisha namna ya kubainisha ishara na dalili za unyanyasaji kihisia, italeta mbinu/mikakati ya jinsi ya kuingilia kati na kumsaidia huyu anayejifunza kutambua huduma kwenye jamii husika ili kupata njia mbalimbali za kuwasaidia  wahanga kupona.