1. Je, Maendeleo ya Kila Jambo Maisha ya Mtoto ni nini, na Taasisi ya HCD ni nini?

Maendeleo ya Kila Jambo katika Maisha ya Mtoto (HCD) hushughulikia mambo/vipengele vyote vya maendeleo ya mtoto, sio jambo/sehemu moja tu. Kwa kuwaongoza watoto kupitia mpango unaowakuza kiakili, kimwili, kihisia-kijamii, na kiroho, wanapatiwa fursa bora zaidi za kushinda vikwazo maishani mwao na kufikia/kupata maisha kamili ambayo Mungu anawatakia.

Kwa kutoa mafunzo tendaji ya kifilosofia na ya kiteolojia, yanayofunza Maendeleo ya Kila Jambo katika Maisha ya Mtoto, Taasisi ya HCD imejitolea kuwaelimisha watu kote ulimwenguni ili waelewe maendeleo ya mtoto ikizingatia vipengele vya kiroho, kiakili, kihisia-kijamii na kimwili vya mtu.


2. Je, ni aina gani za mafunzo/kozi zinazotolewa na Taasisis ya HCD?

Taasisi ya HCD hutoa mafunzo/kozi fupi za kuanzia kwa wakufunzi/watendaji wanaoanza kushirikiana na watoto na mafunzo mengine ya hali ya juu kwa wafanyakazi wanaotaka kuimarisha ujuzi wao wa maendeleo ya mtoto, utendaji na filosfia.


3. Ninajua watu wengine wanaoweza kunufaika na mafunzo ya HCD... je nitawasaidia aje?

Unaweza kuwaalika wajiunge na ForChildren.com na wafaidike na mafunzo/kozi za mtandaoni za bila malipo katika Taasisi ya HCD!


4. Je, ninaweza kushirikiana na Taasisi ya HCD ili nitoe mafunzo mahusui kwa ajili ya shirika langu?

Ndiyo Taasisi ya HCD ingependa kushirikiana na wengine wanaowathamini sana watoto ili kuweka kozi za mafunzo za mtandaoni zinazofaa shirika lao. Kwa mfano, dhehebu la kanisa linaweza kuweka moduli ya mafunzo kuhusu Kuwalinda Watoto kwenye Taasisi ya HCD ambayo wafanyakazi wao wanaowatumikia watoto wanahitajika kufanya. Seminari inaweza kuweka kozi za mtandaoni za kupeana alama kuhusu teolojia ya watoto na jukumu la watoto katika Ufalme wa Mungu. Tungependa kuongea nawe kuhusu kushirikiana ili kutimiza lengo hili! Tafadhali Wasiliana Nasi ili kuanza mazungumzo.


5. Nimetengeneza nyenzo zangu mwenyewe za mafunzo za HCD; ninaweza kuzishiriki hapa?

Ndiyo! Tunawatafuta washirika walio na mipango bora ya mafunzo ya Maendeleo ya Kila Jambo katika Maisha ya Mtoto, teolojia ya watoto na mengineyo. Pakia vifaa na video kwenye ukurasa wa "Discover-Gundua" wa ForChildren.com au Wasiliana Nasi ikiwa unataka kushiriki kozi ya mtandaoni kupitia Taasisi ya HCD.


6. Sijawahi kufanya kozi ya mtandaoni hapo awali. Ninaazia wapi?

Tunafurahia sana kwamba uko hapa! Kozi ya mtandaoni ni njia rahisi ya kujifunza wewe mwenyewe, nje ya darasa. Ukibofya kichupo cha buluu cha katikati kwenye ukurasa wa mwanzo wa Kujifunza, unaweza kuangalia orodha ya kozi zote zinazotolewa kwenye Taasisi ya HCD. Bofya kwenye jina la kozi ili kuifungua na kuanza. Bofya mshale wa mbele ili kuenda kwenye ukurasa unaofuata na mshale wa nyuma ili kurudi kwenye ukurasa wa awali. Kila kozi ina maelekezo ya kina ya uabiri kwa hivyo usiwe na wasiwasi ikiwa ndiyo mara yako ya kwanza Ikiwa uko na maswali yoyote au unahitaji usaidizi, unaweza ku Wasiliana Nasi ili kutuma swali. Timu ya ForChildren inafurahia sana kukuhudumia!


7. Swali langu halikujibiwa hapa. Je, ninaweza aje kupata usaidizi?

Bofya tu kiungo cha Wasiliana Nasi kwenye ukurasa wa mwanzo wa ForChildren.com, kwenye sehemu ya chini kulia. Tuma jina lako, barua pepe na swali kwa kutumia fomu inayojitokeza. Mtu kutoka timu ya ForChildren atawasiliana nawe haraka!

Last modified: Jumanne, 15 Januari 2019, 4:33 AM