Lazima uwe mmoja wa jamii ya ForChildren.com ili upakue rasilimali. Bofya vitufe vilivyo hapa chini ili uingie au ujisajili!
Kategoria | Ulinzi wa Mtoto |
Mmiliki wa Rasilimali | Chrissy Sykes |
Also Available in | English, Spanish, French |
Mwandishi | Chrissy Sykes |
Mafunzo ya Wimbo wa 2 wa Iwapo Huna Hisia Njema Kulihusu yanawatayarisha wazazi na watu ambao wanafanya kazi na watoto kuwasilisha wimbo wa pili kwenye toleo la Mwili Wangu ni Mwili Wangu. Wimbo huu unajadili hisia, shinikizo la rika na kuwaelimisha watoto ili walinde mwili wao. Mafunzo yanajumuisha mwongozo wa majadiliano na shughuli za ziada za kujadili mada zilizotajwa kwenye video. Mengine yaliyopo ni maneno ya wimbo na “Kanuni Rahisi” zinazowasaidia watoto kusikiliza hisia zao, wawe wajasiri na “Wakatae” na waelewe kwamba hawapaswi kunyamaza ama kuweka siri ikiwa mtu anawaumiza.
ForChildren.com, inayotolewa na Compassion International, hutoa mawazo, fursa za kujifunza na uhusiano kuwasaidia watu wanaofanya kazi na watoto walio hatarini. Sisi ni jamii ya duniani kwote ya wafuasi wa Yesu iliyojitolea kwa ukuaji wa watoto wa jumla. Tunakualika ujiunge nasi katika jamii yenye ushirikiano kushiriki mawazo, uzoefu, mbinu na zana zinazowasaidia watoto kuimarika hata wakiwa katika shida.
ForChildren.com inatolewa na Compassion International, shirika lisilo la faidia lililosajiliwa 501(c)3. Nyenzo, kozi, na majadiliano yote yanakusudiwa kwa matumizi ya elimu peke yake, na sio kwa faida.